JMMBA
Kinondoni Municipal Council logo Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A
Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A

Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A

Hii ni sehemu maalum ya taarifa za Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A ndani ya Kata ya Kawe, Manispaa ya Kinondoni. Hapa wakazi wanaweza kuona matangazo muhimu, taarifa za utekelezaji, nyaraka za utambuzi wa wakazi, taarifa za ulinzi shirikishi, na marejeo muhimu yanayohusu maisha ya kila siku katika mtaa.

Ukurasa huu umeandaliwa ili taarifa muhimu zisiwe zinapotea kwenye vikundi au vipeperushi vya muda mfupi. Unakusanya mambo yanayohitaji kuonekana wazi, kupakuliwa kwa urahisi, na kurejelewa tena na wakazi, viongozi wa mtaa, na wadau wa maendeleo.

Tangazo la leo

Usafi wa ufukwe leo na taarifa ya Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri

Leo ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi. JMMBA inaendelea na shughuli ya kawaida ya usafi wa ufukwe wa Mbezi Beach A asubuhi, huku tukiwajulisha wakazi kuhusu maadhimisho ya International Day of Zero Waste ya tarehe 30 Machi 2026. Ujumbe rasmi wa kimataifa wa mwaka huu ni “Zero waste starts on your plate”, ukihimiza kupunguza upotevu wa chakula na taka zinazoweza kuzuilika kabla hazijafika kwenye mazingira yetu.

Shughuli ya leoBeach clean-up ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, Mbezi Beach A, kuanzia saa 12:00 asubuhi.
Taarifa ya NEMCElimu kwa umma kuhusu Zero Waste inaendelea Dar es Salaam kuanzia 28–30 Machi 2026, Mnazi Mmoja Grounds.
Kwa wakaziTafadhali punguza upotevu wa chakula, tenganisha taka kwa uwezo ulio nao, na epuka kutupa taka hovyo kwenye mifereji na maeneo ya makazi.
Mazingira ya leo

Muonekano wa shughuli ya usafi wa ufukwe

Picha hizi zinaweka kumbukumbu ya ushiriki wa leo katika usafi wa ufukwe wa Mbezi Beach A. Zimewekwa hapa kama sehemu ya taarifa ya umma kuhusu shughuli ya leo ya jamii.

Washiriki wakikusanya taka ufukweni
Washiriki wa community clean-up wakifanya kazi ya kukusanya taka zinazoonekana kwenye eneo la ufukwe.
Washiriki na ulinzi shirikishi kwenye beach clean-up
Ushiriki wa wanajamii na ulinzi shirikishi katika zoezi la usafi wa leo.
Vijana wakibeba mifuko ya taka baada ya clean-up
Vijana wakibeba mifuko na vifaa baada ya kukusanya taka katika eneo la ufukwe.
Uhamasishaji wa mazingira

Zero Waste Day 2026 na kampeni ya NEMC

Kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na NEMC, Dar es Salaam inaendesha programu ya elimu kwa umma kuhusu Taka Sifuri kuanzia tarehe 28 hadi 30 Machi 2026 katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Taarifa hiyo imeeleza kuwa maonesho na elimu ya umma yataonesha namna taka zinavyoweza kubadilishwa kuwa malighafi, bidhaa nyingine, na fursa za kiuchumi, sambamba na uhamasishaji wa matumizi bora ya rasilimali na upunguzaji wa upotevu wa chakula.

Zero waste starts on your plate
RethinkRethink
RefuseRefuse
ReduceReduce
ReuseReuse
RepairRepair
RegiftRegift
Recycle and compostRecycle & Compost
Taka Sifuri 2026
Taka Sifuri 2026

Ujumbe wa uhamasishaji wa kitaifa kuelekea 30 Machi 2026.

Taka ni fursa
Taka si uchafu tu

Elimu ya kuona taka kama fursa ya uchakataji, ajira, na bidhaa mpya.

Taarifa ya awali

Taarifa ya awali: mkutano wa wakazi kuhusu mradi wa majitaka

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A, akishirikiana na Mkandarasi wa Mradi wa Majitaka (BCEG) pamoja na DAWASA, anawakaribisha wakazi wote kwenye mkutano wa wakazi utakaofanyika Jumamosi tarehe 14/3/2026 saa 3:00 kamili asubuhi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A.

Ajenda 1Kupokea taarifa ya Mradi wa Majitaka.
Ajenda 2Changamoto na kero za mradi.

Wananchi wote mnakaribishwa.

Mambo yanayopaswa kuonekana wazi

Mpango wa ulinzi shirikishi wa Mbezi Beach A

Mpango wa ulinzi shirikishi wa mtaa umegawanywa katika kanda saba: Kanda D, Kanda E, Kanda F, Ukanda wa Bahari Kaskazini, Ukanda wa Bahari Kusini, Makazi Mapya, na Capt. Komba. Idadi ya walinzi imeongezwa na itaendelea kuongezwa kulingana na mahitaji ya kiusalama yatakayojitokeza.

Barriers zitawekwa kwa awamu kulingana na mwitikio wa uchangiaji. Kwa makazi, kiwango cha uchangiaji ni TZS 20,000 kwa mwezi. Kwa maeneo ya biashara, kiwango ni kuanzia TZS 50,000 mpaka TZS 100,000 kutegemeana na aina ya biashara.

Makundi / kampuni zilizopitishwa

  • Mswiha Security Company Ltd — Block D
  • Muzakir Group Investment — Block E
  • Nyota Security Group — Wakazi wa Block F na J
  • Kikundi cha Polisi Jamii — Ukanda wa Bahari Kaskazini na Kusini

Kila mkazi anatakiwa kuweka taa kwenye fence na kufyeka vichaka vilivyo pembezoni mwa nyumba. Ukaguzi utafanyika mara kwa mara na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka maelekezo.

Malipo ya ulinzi shirikishi
CRDB: 01330003LRC01 Jina la akaunti: SERIKALI YA MTAA MBEZI BEACH A - TOZO Malipo yafanyike kila tarehe 25–27 ya mwezi husika ili walinzi walipwe kwa wakati.

Fomu ya kutambua wakazi

Fomu hii inakusanya taarifa za mmiliki wa jengo, anayekaa, na wanakaya wote. Ikiwa nafasi haitoshi, taarifa zinaweza kuambatanishwa kwenye karatasi nyingine na kuwasilishwa ofisini au kwa WhatsApp.

WhatsApp: Simon Kivambe 0694 240210 • Ramadhani Atuman 0748 018041
Email: e.mwamyalla@hotmail.com

Pakua fomu ya wakazi

Kamati za Serikali ya Mtaa

Serikali ya Mtaa imeunda kamati za ulinzi, ujenzi na miundombinu, afya na mazingira, elimu na malezi, fedha na mipango, ustawi wa jamii, pamoja na michezo, burudani na utamaduni ili kusimamia majukumu ya maendeleo kwa ufanisi.

Pakua taarifa ya kamati

Mradi wa majitaka

Faili hili linaorodhesha mitaa au nyumba ambazo hazijafikiwa na mradi wa maji taka. Ni rejea muhimu kwa wakazi wanaotaka kuthibitisha hali ya eneo lao kabla ya kufuatilia kwa ofisi husika.

Pakua faili la mradi wa majitaka
Pakua nyaraka

Nyaraka muhimu za Serikali ya Mtaa